NDOTO YAKO NI IPI?

Tunaweza kuota kuwa watu wenye mafanikio maishani. Hasa kwa njia ya kujiajiri wenyewe. Lakini uzoefu wa kujisimamia mwenyewe katika biashara unaonesha kuwa mtu anahitaji kuelewa mambo ya msingi ambayo lazima akumbane nayo ili kusonga mbele. Na kama tukitenda kwa usahihi basi tuna nafasi kubwa ya kufanikiwa. Na kwa hakika ujasiriamali unahitaji mtu mwenye nia na utayari wa mafanikio kiasi kwamba siku moja atapata nafasi ya kuingiza pesa ambayo hapo awali ilikuwa ndoto tu.

Wajasiriamali vijana wenye mafanikio ni wale ambao wana mawazo ya ubunifu yaletayo ideas mpya za biashara. Kuwa na fikra bunifu hakuleti mafanikio mpaka mtu atakapofanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa fikra hizo zinatekelezeka. Lazima mtu afanye utafiti wa kina. Lazima ahakikishe kuwa fikra yake mpya inauzika sokoni. Na jambo la mwisho mjasirimali anahitaji kujiamini, nyezo na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kupambana na chagamoto zinazojitokeza mbele.

Mjasiriamali lazima aelewe kwamba mafanikio yanaweza kuchukua miezi na hata miaka kadhaa kuonekana. Uvumilivu unahitajika na mawazo ya kukata tamaa hayatakiwi.

Mjasiriamali mwenye kiu ni lazima azungume na watu wanaoweza kumsaidia katika biashara au wazo lake na ni lazima afanye utafiti wa maoni (surveys) na kusoma vitabu vinavyohusiana na aina ya biashara anayotaka kufanya. Hii inamsadia kufahamu undani wa biashara anayoihitaji na hata matamu na machungu ya kuwa mjasiriamali muwajibikaji.

Pale mjasiriamali anaporidhika na taarifa alizozikusanya juu ya wazo la biashara yake, hatua inayofuata ni kuwa na vitendea kazi au nyenzo zitakazomuwezesha kuchukua hatua ya kwanza ya utendaji. Mara nyingi fedha inakuwa ni nyezo ya kwanza katika utekelezaji. Fedha hii inaweza kuwa ni ile iliyotunzwa kwa ajili ya wazo husika. Na kama hakuna fedha basi mabenki yanaweza kufadhili wazo la biashara. Au pia inawezekana kupata fedha kwa kutafuta mshirika wa biashara (business partner)

Baada ya biashara kuwa imeanza swala linalofuata kwa mjasiriamali ni kupata wateja. Mjasiriamali mchanga lazima afahamu kwamba wateja ni muhimu sana katika kuifanikisha au kuiua biashara yake. Kupata wateja wanaoamini bidhaa au huduma ya mjasiriamali ni hatua muhimu sana. Kama bidhaa au huduma inayotolewa ni yenye kiwango cha juu, na kama wateja wanapata kile wanachoahidiwa basi swala linakuwa ni namna gani biashara ikue.

 
 

Hivyo mjasiriamali analazimika kuweka sera madhubuti ya biashara yake ili kuifanya ikue na kuendelea kuvutiwa wateja.

Kwa kawaida hamasa ya mafanikio kwa wajasiriamali vijana inatokana na watu maarufu waliofanikiwa katika kundi la biashara wanazotaka kufanya. Wajasiriamali vijana wenye maono ya mbali huelewa kwamba hata watu maarufu ambao wanataka kuwaiga walianza chini kabisa. Hii huwapa morali na ngvu ya kusonga mbele. Baadhi ya watu maarufu waliopata mafanikio ni kama vile Thomas Edison, John D Rockefeller, Andrew Carnegie, Henry Ford, Bill Gates, Walt Disney, Richard Branson, Donald Trump, na Ted Turner kwa uchache wao.

Watu wenye mafanikio makubwa katika biashara walianza kama mjasiriamali kijana anayeanza kwa kuwa na wazo kubwa na hamasa na nidhamu ya hali ya juu ya kuweza kujisimamia. Watu hawa walifikiri juu ya biashara waliyotaka kuifanikisha, wakafanya kazi usiku na mchana, wakajitolea kwa kila hali na zaidi ya yote waliamini juu ya kile walichotaka kukifanikisha.

Watu hawa wakubwa duniani ambao wanaheshimika na kuenziwa na ambao ni matajiri waliopindukia walianza kama wewe wakiwa vijana wadogo wenye ndoto za mafanikio. Walikuwa na tamaa na uvumilivu wa kusonga mbele mpaka wakafanikiwa. Kwa hivyo hakuna sababu zozote kwamba vijana wa siku hizi ambao pia wana ndoto za kufanikisha kile wanachoamini hawawezi kuwa kama majabari haya.

Labda pengine jina lako linaweza kuwa miongoni mwa orodha ya watu wakubwa na maarufu duniani katika miaka michache ijayo. Nani anajua?!


Asante kwa kuwa pamoja na mimi.

Wasiliana nasi kwa maoni au ushauri zaidi

Pius Justus Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *