NAMNA YA KUISHI KWA KUJIWEKEA AKIBA (SAVINGS) ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO BINAFSI

©Eskimi
1. Epuka kununua vitu bila mpangilio usioelewaka.
 Mfano sisi wanaume unaweza kununua viatu vichache vyenye ubora ili fedha yako uipeleke kwenye malengo yako.

2. Epuka kushindana na fashion.
Unaweza ukajiwekea kipindi maalumu cha kufanya manunuzi ya nguo na vitu vingine ambavyo vinaendana na hivyo.

kutaka kila nguo nzuri inayotoka na ili kuonekana nayo, hii tabia itakufilisi mapema na matokeo yake utaanza kuishi kwa kukopa kopa na utaishia kwenye utapeli na wizi ili uwa-impress watu.

3. Epuka kutumia kiasi kikubwa kwenye simu kwa shughuli ambazo sio productive.
 Mfano unanunua vifurushi vya hela kubwa vya wiki au mwezi kisa unachat tu na marafiki kupitia fb, WhatsApp, Twitter, Viber etc. ili mradi na wewe uonekane while unajua hiyo hela uliyotumia haiturudi kwa faida. Weka fedha kidogo tena kwa mawasiliano muhimu na ya maana. Punguza sifa zisizo na tija.
4. Epuka tabia ya kukopa benki au kwenye taasisi nyingine za kifedha pasipokuwapo na malengo.
 Mfano unakopa benki ukanunue Iphone 6, ili na wewe uonekane umo. Utafilisika na utaanza kuabika. Fanya vitu kwa malengo huku ukijua utamudu hayo malengo.
5. Epuka kutembea na hela nyingi kwenye wallet na sehemu zinazofanana na hizo.
 Maana ukiwa na petty cash nyingi mfukoni kwa wakati mmoja unatengeneza tabia au mazingira ya kuweza kutumia fedha hizo hovyo bila mpangilio.Tembea na kiasi cha fedha unachojua una matumizi nayo kwa wakati husika.
6. Hakikisha unakuwa na timetable ya kudumu ya maisha yako kwenye kila jambo.
 Epuka kuishi kama bendera kwamba upepo ukija huku unakupeleka na ukienda kule unakukimbiza. Jifunze kwa taratibu then utaanza kuona mabadiliko kwa utaratibu yanakuja na utaona unapiga hatua kwa haraka na wepesi zaidi.

Asante kwa kuwa na mimi.
wasiliana nasi kwa;

Pius Justus Muliriye
0754745798 – Whatsap
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *