Habari rafiki yangu na msomaji wa makala zangu katika mtandao huu.
karibu tena kwenye makala zetu hizi za kila siku.
Natambua kila mtu yuko bize sana katika harakati za kubadilisha maisha yako kuwa bora zaidi. Nikutie moyo tu ndugu nyangu, endelea kupambana na endelea kujifunza kila siku, soma sana vitabu, pia jitahidi sana kutembelea mtandao huu ambao utakupa hamasa kubwa ya kuanza hata kama umekata tamaa.
Leo naomba nikushirikishe mambo muhimu sana ambayo yatakusaidia kusonga mbele.
Hizi ndio njia muhimu sana ambazo zitakusaidia kufikia malengo yako;
- Jua Unachotaka kutimiza.
kila mtu ana malengo yake katika kutimiza kile anachokitaka, ni jambo jema sana uweze kujua unataka kutimiza nini katika maisha yako, nini lengo lako?
kuna usemi unasema; “a goal is not a goal until its entered on paper” ikiwa na maana kwamba “Lengo sio lengo mpaka liwekwe katika maandishi na kupewa muda wa kuweza kulitimiza”
Ukiwa na lengo huwa lina tabia ya kuchora picha kichwani na unaona huna ulazima wa kuliandika ukijua utalikumbuka, kumbuka kuna mambo mengi sana unayawaza, pia kuna mambo mengi unakutana nayo, haya yote yatakufanya usahau kabisa lile lengo lako kuu, na ndio maana nakusihi kuandika katika notebook yako ili iwe rahisi kukumbuka.
Pia ni lazima uweke muda (deadline) wa kutimiza lengo lako hilo, kwa mfano, una lengo la kujenga nyumba, tengeneza ramani ya nyumba yako, weka picha hiyo ukutani nyumbani kwako sehemu ambayo itakuwa rahisi kuona mara kwa mara hasa hasa chumbani kwako, hii itakusaidia kukumbuka lengo lako hilo na hatimaye kukusukuma kulifanya na hatimaye kutimiza lengo lako.
- Jiulize kwa nini kuna umuhimu wa kuweza kutimiza lengo hilo.
ukiweza kujua hili, kwanza inakuongezea hamasa na ari ya kuweza kupambana na kutimiza lengo lako, na jinsi hamasa inavyozidi kuongezeka ndio unajiweka karibu na mafanikio yako. hii itakufanya kujua kusudi lako lina kitu gani ndani yako.
- Fikiiria katika kutimiza ndoto yako unadhani ni changamoto gani ambazo unaweza kukumbana nazo.
katika maisha, ni jambo jema sana kuwaza juu ya changamoto ambazo unafikira zinaweza kuathiri utekelezaji wa ndoto au malengo yako.
kuna usemi unasema ” Even persons with positive thought have negative thought but, they don’t allow to be part of their life”
ni vyema sana kuziandika changamoto hizo ili utafute ni jinsi gani utaepukana nazo au ni jinsi gani ya kuweza kuzikabili. Tafuta watu ambao wanaweza kukusaidia kuepukana au kukusaidia pindi pale changamoto hizo zitakukabili.
“Kumbuka, ni vyema kujiandaa na changamoto usikutane nazo kuliko kutojiandaa na ukakutana nazo na zitakuharibia lengo lako.”
- Jifunze kutoka kwa watu wanaofanya kitu ambacho unataka kufanya.
Katika kufikia ndoto zako ni vyema sana ukatafuta taarifa muhimu sana kuhusu kile unachotaka kufanya. Tafuta taarifa kutoka kwa watu ambao wanafanya tayari kitu ambacho unataka kufanya, hii itakufanya ujue ni njia gani ufate ili ufanikiwe zaidi, pia itakusaidia kuepeuka changamoto fulani ambazo wao wamepitia na hatimaye kufikia lengo lako.
Jitahidi kusoma kila siku juu ya kitu unachotaka kufanya, si kila kitabu kinafaa kusomwa, be specific, kama ni biashara, soma kuhusu biashara, kama ni mahusiano basi soma kuhusu mahusiano.
Katika vitabu kuna siri nyingi sana zimefichwa huko, lakini wanaosoma ni wachache sana na ndo maana wale wanaosoma hufanikiwa zaidi kuliko wale wasiosoma kabisa.
- Andika mikakati ya matendo katika kutimiza lengo lako.
Baada ya kuweka malengo yako na umejiifunza kutoka kwa watu wengine basi unatakiwa kujiwekea mikakati na mbinu za kufata ili kutimiza malengo yako.
Hii ni kanuni ambayo anaitumia Dr. Peal na naamini itakusaidia kama utaweza kuitumia vizuri.
Dr. Peal anasema, ili ufikie malengo yako ni lazima ujiulize maswali haya matatu;
- Wapi (where) = Wapi unataka kufika na malengo yako?
- Lini (when) = Lini unataka kufika sehemu ya malengo yako?
- Nini (what) = Nini ambacho utafanya kuweza kufikia malengo yako (Action Plans
Nafikiri umeweza kupata chochote katika makala haya ya siku ya leo. Napenda nikutakie utekelezaji mwema wa kutimiza malengo yako kwa kufuata hatua hizo, naamini utafanikiwa tu.
asante kwa kuendelea kuwa na mimi. Nakutakila kila lakheri;
Kwa mawasiliano zaidi;
Pius Justus Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com