Habari rafiki,
natumaini unaendelea vizuri na maisha yako. nikushukuru wewe unayeendelea kufatilia makala haya kila siku hapa kwenye mtandao wako wa www.shuletanzania.info. Nikutie moyo tu, uko mahali sahihi kabisa.
Leo napenda kuanndika na kukushirikisha kuhusu Watoto wetu.
Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu watoto wao kuwa na tabia mbaya kwa kuwwa na utovu wa nidhamu, napenda kukusihi tu, kwamba usilalamike, nitakwambia ni kwa sababu gani usilalamike.
Tusilalamike kuona watoto wanatumia simu muda wotena tukaanza kuwachapa, ila tutumie huo udhaifu wa watoto kwa kuweka kwenye simu vitu vya kuwaendeleza,
Mfano; mwekee Application ya VITABU kwenye simu hiyo, au kama anapenda Tv sana, usimuondoe kwenye TV ila mweke chini ongea naye kuhusu hasara za chaneli ambazo anaangalia. Ukiona mtoto anapenda sana kucheza mpira kuliko kusoma usimpige aache ili asome, hapana, kaa naye muelekeze ka5ti ya mpira na kusoma umuhimu wake na hasara zake (ila angalia kama ni kipaji chake usije ukakiua)
Nazungumza na taifa hili ambalo tunataka kubadili watu lakini mbinu za kuwabadilisha ndizo tunakosa, naongea na wazazi ambao wanataka watoto wao kuja kuwa watu wakubwa lakini wanawaandaa katika mazingira ya kuwa watu wa chini!
Naongea na mzazi kuwa hakuna mtoto ambaye hana akili hata kama bado hajaanza kuongea na wala asikudanganye mtu kwamba mtoto akianza kuongea hapo ndipo akili inafanya kazi ili kuanza kumfundisha. Achana na hizo dhana za zamani za ukila mayai kama ni mjamzito mtoto atatoka na kipara au utashindwa kujifungua.
Kama unampenda mtoto wako na kila siku unamwambia maisha ni magumu basi usimpitishe katika njia ambayo hata wewe umepita, usihangaike kumuwekea mtoto waako akiba benki, ukaacha kumwekea mtoto wako akiba katika akili yake kwa kuanza kununua vitabu taratibu na kutengeneza Home Library.
Mtoto hata kama akishika kitabu ambacho hakielewi utamjenga kuwa na tabia ya kupenda kusoma kwa baadae tena akiona mama au baba yuko na kitabu ndio kabisa naye atang’ang’ania kusoma ili kuona unachokisoma, na kwa namna hiyo atakutana na maarifa yatakayomsaidia.
Maisha mazuri hayatengenezwi kwa kuanza kuwapeleka shuleni, bali yanaanza kuwalisha mwenyewe vitu tofauti na darasani. Mafanikio ya mtoto wako baadaye hayatengenezwi na degree au masters ambayo mwanao atakuwa nayo.
Mpendwa mzazi au mlezi unapenda kuona maisha ya mwanao kama watu wengine na kutosheka? Unataka mwanao kuwa wa tofauti? kama kweli unataka awe wa tofauti badilisha hii mitazamo katika maisha yake.
Asante kwa kuwa na mimi mpaka sasa, naamini utakwenda kumlea mwanao katika misingi hii.
Ni vibaya sana kutokumpa mwanao maarifa ya kujitambua halafu yeye akaja kujitambua ataona wazazi mlikuwa hamjitambui.
Hatuwezi kuimba wimbo huu wa umaskini kila siku na kiitikio chake kikiwa ni kuua ndoto za watu hasa kuanzia utotoni.
Ndugu mzazi au mlezi mtoto hata akianza kutembea au ukianza kujielewa hata ukimwita basi ni wakati wa kumjenga . Hujawahi kujiuliza kwa nini mtoto akianza kuongea anajuaje hiyo lugha? Ni kwa sababu anasikia toka alipokuwa mdogo.
Asante sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Naomba kwa leo niishie hapa.
Kama umevutiwa na makala hii tafadhari usiache kushea na wenzako, bonyeza facebook icon hapa chini na uwashirikishe wengine. ASANTE.
kwa ushauri zaidi wa mambo kama haya hasa ya kisaikolojia kwa watoto na maswala yote ya kujitambua katika maisha usisite kuwasiliana na mimi kwa mawasiliano yafuatayo;
Pius Justus Muliriye
0754745798 – Whatsapp
0657128567
piusjustus28@gmail.com