USIISHI MAISHA YA WENGINE

Habari rafiki yangu,
karibu katika mwendelezo wa makala zetu za kila siku zinazoendelea kukuhamasisha na kuboresha maisha yako na yangu pia.
Nianze kuelezea suala hili kwa kunukuu usemi wa kiingereza unaosema “The only who can be the best is the one inside you and the one yo see in mirror”

Ikiwa na maana ya “Mtu pekee ambaye anaweza kuwa vizuri zaidi ni yule aliye ndani yako na yule ambaye ukiangalia kwenye kioo unamuona”

Thamani yako haiwezi kuongezeka ukiishi maisha ya watu wengine , na maisha yako hayawezi kuwa mazuri kwa kujilinganisha na wengine.
Thamani yako iko ndani yako, hauwezi kuikuta thamani yako kwa mtu mwingine bali unaweza kuionyesha thamani yako kwa mwingine. Tunatakiwa kujikubali kwa yale machache ambayo tunayo ili tusiyapoteze. Unapolinganisha kidogo ulicho kuwa nacho kwa wengine ndivyo unavyozidi kukipoteza ulichonacho.
Jambo la msingi ni kuangalia jinsi ya kutumia kidogo ulicho nacho kupata unachohitaji.
kujisahau kwetu ni kuamua kufuata maisha ya watu wengine kwa kudhani kwamba maisha yako yatanyooka pasipo kuzingatia nafasi yako ni sawa na kukata mikono yako na kuweka mikono ya bandia kuepuka maumivu. 
dunia haihitaji wewe kutamani kuwa mtu ambaye tayari ulimwengu ushajua uwepo wake, Dunia inakuhitaji wewe kuonesha uwezo wako ambao bado wengi hawajaugundua sio wewe kutumia uwezo wa mwingine kuoonesha kisicho chako.  Nani atachukua nafasi yako kama wewe huhitaji wala hutaki kuonesha uwewe ambao unatakiwa kuishi. 


Asante kwa kuwa na mimi mpaka hapa, naamini umejifunza kitu. kama makala hii imekupendeza, weka maoni yako hapa chini na pia unaweza kuwashirikisha wengine kwa kubonyeza kitufe cha facebook hapa chini ili nao wanufaike na elimu hii.
KARIBU SANA.


Wasiliana nasi;
Pius Justus Muliriye 
0754745798 – Whatsapp
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *