TUMIA MAWAZO HASI KAMA CHANGAMOTO YA KUBADILIKA

Mawazo HASI ni kama meli inayozama, usipoondoka ndani yake unazama nayo. Tumia mawazo hasi kama mtaji wa kubadilika. Mpaka sasa watu wengi wamefungwa na mawazo hasi  yaliyorithiwa vizazi na vizazi na imewapelekea kudhani kuwa wao ndio mawazo hasi na mawazo hasi yanachowaambia hudhani wao ndio wanaowaza.

Nakuhakikishia mawazo hasi huna uhusioano nayo bali umeyarithi kwenye jamii na yakafanikiwa kukudanganya kwamba ni sehemu yako.
mawazo hasi yameendelea kuwatesa watu kwa kuleta maumivu ya kihisia, kuchanganyikiwa kukudanganya kwamba ni sehemu yako.
Mawazo hasi yameendelea kuwatesa watu kwa kuleta maumivu ya kihisia, kuchanganyikiwa, migogoro, vurugu, magonjwa, kukata tamaa, chuki, hasira, hofu na mambo yanayofanana na hayo.
Naposema tumia mawzo hasi kama mtaji wa kubadilika nakumbuka hadithi moja maarufu. Hadidhi hiyo inasema

“Mwana mpotevu aliomba urithi kwa baba yake na akaondoka akaenda nchi ya mbali, kisha akatumia mali yake ya urithi kwa uasherati – Njaa ikaingia nchi ile na akawa hana mtu wa kumpa kitu tena. akazingatia moyoni ni watumishi wangapi aliowaacha kwa baba yake wanakula na kusaza. Akaamua kurudi kwa baba yake na kuomba msamaha na kuwa mwana mwema. Baba yake alimwona,akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. Pia baba yake aliwaambia watumwa wake, letieni upesi vazi lililo bora, mkamvike, mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni. Mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia “HUO NDIO UPENDO WA MUNGU KWA WATU WAKE” na haijalishi ukoje.

Hivyo basi inawezekana kabisa kuachana na mawazo hasi na kuwa watu huru . Tunapaswa kuishi kwa kumtegemea Mungu na sio akili zetu. Pia Mungu anatupenda sana bila kujali tulivyo LA MSINGI Jifunze kuachilia mambo yaliyopita na pia achana na kuwaza sana kesho kwa sababu hakuna ajuaye kesho. Ukishaweka mipango usihangaike na matokeo, matokeo yatajishughulikia menyewe.

Pata kopi yako ya kitabu ambacho kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani kama Sabuni za mche, sabuni za maji, sabuni za kusafishia chooni (disfectant), batiki, na bidhaa nyingine nyingi. Kitabu hicho kipo katika mfumo wa SOFTCOPY (nakala laini) ambayo unaweza kusoma kwenye simu yako, utatumiwa kupitia whatsapp au email. Utapata kitabu hicho kwa Tsh. 5000/- tu. Utalipia kwa MPESA 0754745798 au TIGOPESA 0657128567 – PIUS MULIRIYE. KARIBU.

Wasiliana nasi?

Pius Muliriye Justus 
0754745798-WhatsApp 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 
www.shuletanzania.info 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *