MICHELLE OBAMA ANAKUPA SOMO LA KUWEZA KUFANIKIWA!

Kipindi kigumu cha kutokuwa na fedha…

Unapokatiza mitaani katika kona mbalimbali nchini, kilio cha wengi ni kwamba wapo kwenye kipindi kigumu cha kutokuwa na fedha mifukoni kwa sababu mbalimbali. Watu wanasema serikali imeamua kuwanyoosha ili watu wawe na nidhamu ya matumizi ya fedha.

Lakini wakati unapojiuliza namna ya kutoboa unaweza kupata somo zuri la mafanikio kuka kwa Michelle Obama, mke wa Rais Barack Obama wa Marekani anayeelekea kumaliza muhula wake wa pili wa urais ili kumpisha aliyechaguliwa hivi karibuni, Donald Trup atakayeapishwa baadaye mwezi ujao.

Unapomtaja Michelle, unataja mwanamke mweusi aliyeweka historia ya kuingia ikulu akiwa kama mke wa Rais Obama.

Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 52 ni mwandishi na mwanasheria ambaye alichukua digrii yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani kati ya mwaka 1985 hadi 1988 kabla ya kuolewa na Rais Obama mwaka 1992 na kubahatika kupata watoto wawili, Malia Ann na Sasha.

SOMA: KITABU CHA JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MCHE, SABUNI ZA MAJI, CHAKI n.k

Baada ya kuingia ikulu kama mke wa rais wa 44, Michelle anaweka wazi mbinu mbalimbali zilizomfanya kufanikiwa hata kabla hajaingia ikulu kiasi cha kuwa na utajiri wa Dola milioni 11.8 (zaidi ya shilingi bilioni 23) ambao ni zaidi ya mumewe mwenye utajiri wa dola milioni 4 (zaidi ya bilioni 8). Baadhi ya mbinu hizo ni kama zifuatavyo;

USIANGALIE ULIPOTOKA, SONGA MBELE

Kwenye masomo yake kuhusu mafanikio Michelle anasema kuwa: “Watu wengi wamekuwa wakikata tamaa mara baada ya kuona hali ni ngumu (kama ilivyo nchini kwetu kwa sasa) ambao hawakufanikiwa kwa kile walichokipanga kabla. “Inawezekana walipata fedha nyingi lakini baadaye wakafilisika kama ilivyokuwa kwa Henry Ford, Walt Disney na wengine wengi. Hutakiwi kukata tamaa, hutakiwi kusema kwamba huo ndiyo mwisho kwani hata watu hao walivyofilisika, wakajitafakari na baadaye kutajirika tena kama ilivyokuwa.”

FANYA KAZI KWA BIDII

Michelle anasema: “Njia kuu ya kufanikiwa ni kufanya kazi kwa bidii. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kuna wakati baba yangu alikuwa akiumwa sana. Wakati mwingine mama alimwambia kwamba hakutakiwi kwenda kazini lakini hakukubali, alikuwa akiamka asubuhi na mapema na kwenda huko kwani aliamini katika kufanya kazi kwa bidii.
“Huwezi kufeli kama kweli utaamua kufanya kazi unayoipenda kwa bidii.”

USIOGOPE KUFELI

Michelle anaendelea kukufundisha: “Unapofeli ndiyo unapata nguvu ya kufanikiwa zaidi kwani itakufanya kujiuliza ni wapi ulipoanguka? Wengine hawataki kujaribu kwa kuwa wanaogopa kufeli. Hutakiwi kuogopa kufeli ili ufanikiwe, wakati mwingine unatakiwa kufeli.”

PANGA UNATAKA KUWA NANI

Michelle: Unatakiwa kuendelea kupambana na lengo lako la kujua unatakiwa kuwa nani kwenye maisha haya. Unapopata jibu, ni lazima ufanye yale magumu ambayo yataonekana kuwa vigumu kutokea.

“Unapoamua kufanya magumu yatakufanya kukomaa na hata yakija yale mepesi utaweza kuvuka kirahisi sana. Usitake kujifananisha na mtu mdogo, ni lazima ujifananishe na mtu mkubwa ili upambane zaidi. Kama unahisi huwezi kuwa kama Bill Gates, sasa inuka na useme kwamba unataka kuwa zaidi ya Gates.”

FURAHIA MAISHA

Pamoja na ugumu wa aina yoyote unaopitia lakini Michelle anakuambia: “Unatakiwa ufurahie maisha. Usitake kufanya kazi tu mwaka mzima bila kupumzika. Wakati mwingine unapomaliza kazi zako na kufanikiwa, yafurahie maisha, sikiliza muziki, angalia televisheni kwa ajili ya kuupumzisha mwili wako, hata inapotokea kufanya safari fulani kwenda kujifunza, nenda, hakikisha unayafurahia maisha baada ya kazi ngumu, itakusaidia sana kupunguza msongo wa hali ngumu kimaisha.”

SOMA: KITABU CHA JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MCHE, ZA MAJI, ZA UNGA, CHAKI n.k

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *