Habari mwana familia wa PM PROJECTS, natumaini unaendelea vizuri na harakati za kukomboa maisha yako.
Leo hii tutajifunza ni jinsi gani ya kutengeneza sabuni za mche kwa njia rahisi kabisa.
Kabla ya kuendelea tutaangalia mahitaji muhimu yanayohitajika katika kutengeneza sabuni hizo.
- Mafuta ya kula (yenye uwezo wa kuganda)
- Cautic soda
- Maji baridi
- Sodium silcate
- Rangi (unayopenda)
- Perfume (kama ukipenda)
Hayo ndio mahitaji muhimu sana katika kutengeneza sabuni za mche zenye ubora wa hali ya juu kabisa.
Sabuni za mche ni bidhaa ambayo ni muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani inatumika karibia kila siku. Kuanzia asubuhi unapoamka na unapomwenda kulala.
Kwa maana hiyo, sabuni hizi zina soko kubwa sana na soko lake haliwezi kuisha leo wala kesho. Kwahiyo kama wewe umeamua kuwekeza katika uzalishaji huu basi umechagua bidhaa muhimu sana na utafanya biashara maisha yako yote.
Baada ya kufahamu hayo, tafadhari endelea kutembelea blog hii kwa sababu makala ijayo tutaonyesha njia unazotakiwa kufuata wakati wa kutengeneza sabuni hiyo ya mche.
Asante kwa kuendelea kutembelea blog yetu hii.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;
PIUS JUSTUS MULIRIYE
Whatsapp – 0659908078