MAMBO MATATU (3) YA KUFAHAMU KABLA YA KUWA MJASIRIAMALI WA MTANDAO.

Habari rafiki, nafurahi kuwa pamoja na wewe siku ya leo tena ambapo ninakwenda kushea  na wewe mambo ya msingi sana unayotakiwa kuwa nayo kabla ya kuwa mjasiriamali wa mtandao.

Kabla ya yote jana nilirusha video iliyokuwa inaonyesha jinsi nilivotumia mtamdao wa internet kutengeneza hadi million 7 na zaidi kupitia mtandao wa internet, kama hujaiona nitakuwekea mwisho wa makala hii uweze kuitazama.

Tuendelee na mada yetu ya siku ta leo, mada inasema mambo matattu ya msingi ya kufahamu au ya kuwa nayo kabla hujaanza kuwa mjasiriamai wa mtandao.

Mjasiriamali wa mtandao maana yake ni kwamba, mtu au kampuni inatoa huduma au bidhaa kupitia mtandao wa internet.

Mambo hayo ni:-

1. WAZO (TATIZO LA KUTATUA.)
Hii ni moja ya kitu muhimu sana mtu yeyote anayetaka kuingiza pesa kupitia mtandao anatakiwa awe nayo. Ni lazima uwe umeabaini tatizo linaloisumbua jamii na una njia ya kuweza kulitatua, kama huna huwezi kutengeneza hata senti moja mtandaoni, nitakushauri uendelee kuchati tu kama wanavyofanya wengine.

2. MPANGO
Baada ya kuwa na wazo au umebaini jamii iliyoko mtamdaoni ina tatizo gani weka mpango thabiti wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Hili ndio jambo muhimu kabisa kwani hapa unaandaa mikakati ya kuweza kusaidia tatizo hilo kabla hujajitokeza mtandaoni na kutangaza.

Mpango unaweza kukusanya taarifa sahihi za jinsi ya kutatua tatizo hilo (HOW TO…) baada ya hapo unaweza kwenda kifua mbele na kujibrand sasa mtandaoni na pesa zitakufuata tu.

3. JUKWAA (PLATFORM)
Hapa ndio kuna pesa, kama huwezi kujenga jukwaa basi hata kama una wazo zuri, au umeandaa mpango mzuri bado hutaweza kuingiza chochote, kwani jukwaa ndio kitu cha msingi sana.

Jukwaa hujengwa kwa utaratibu maalumu ambao unatakiwa ujifunze ni jinsi gani utaweza kujenga jukwaa ambalo litaweza kukulipa maelfu ya pesa.

Jukwaa linaweza kuwa FACEBOOK MESSENGER BOT, YUTUBE CHANNEL AU WHATSAPP GROUP, majukwaa hayo kuna utaratibu wa kuweza kuyajenga na yakakuletea tija. Hili ni somo refu sana na unatakiwa ujifunze kwa kina.

Baada ya kuwa na vitu hivyo muhimu sasa unaweza kuingia mtandaoni na utatengeneza pesa nyingi sana.

Tambua kuwa huduma za mtandao Tanzania inakuwa kwa kasi kubwa sana, watu wengi wapo kwenye mitandao ya kijamii na kila mtu ana matatizo yake na wanahitaji kujua jinsi ya kuyatatua, nani wa kuweza kuyatatua??? Jibu sahihi ni wewe na si mtu mwingine.

Baada ya kusema hivyo mimi kama mmoja wa watu wachache wanotumia mtandao vizuri kibiashara nimeanzisha darasa la kufundisha vijana wenzangu wanaopenda kutumia mtandao kwa tija kujiingizia kipato na kwa njia halali kabisa, darasa hilo litakuwa kwenye group ya whatsapp, kama unataka kujifunza basi unakaribishwa, bonyeza picha hii chini kuingia darasani, wahi sasa nafasi ni chache.

Pia kama nilivyokuahidi kukuwekea ile video, kama hujaisikiliza unaweza kufanya hivo hapa chini.
Asante kwa muda wako, tukutane darasani.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;
Pius J. Muliriye
0717375782|whatsapp only
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *