Katika mfululizo wa mada zetu juu ya jinsi ya kutumia mtandao wa internet kibiashara leo hii ninakuletea mada inayozungumzia Saikolojia ya watu walioko katika mitandao ya kijamii.
Kama tunavyojua, katika mitandao ya kijamii ni sehemu ambako watu hukutana na kujumuika pamoja, kuchati, kuonyesha style mbalimbali za maisha, kwa kulitambua hilo ninapenda kukwambia rasmi kuwa katika mitandao ya kijamii SIO MAHALI PA KUUZIA BIDHAA YAKO AU SIO MAHALI PA KUFANYIA BIASHARA YAKO.
Hii ni sawa na kuwakuta watu wako katika club wanacheza mziki na kuponda raha halafu wewe unaingia na bidhaa zako na kuanza kuwatangazia ili wanunue, nakuhakikishia watakufukuza na hata kukupiga kwa sababu unawaharibia starehe zao.
Kwa hiyo, kama wewe umekuwa ukiweka picha za bidhaa zako kila mahala kwenye mitandao ya kijamii acha mara moja tabia hiyo.
KAMA NDIO HIVYO, NINI UFANYE??
Badala ya kupost picha za bidhaa na kuwatangazia watu wanunue, tengeneza JUKWAA LAKO/KIJIWE CHAKO na huko ndiko utumie kuwaelimisha juu ya umuhimu wa bidhaa unayoitoa na kisha uwauzie, itakuwa rahisi kununua kwa sababu wameshapata elimu juu ya hiyo bidhaa kutoka kwako. Hivyo ndivo unapaswa kufanya.
JUKWAA NI NINI??
Jukwaa katika biashara ya mtandao ni sehemu maalumu ambako unatumia kuwaelimisha watu kuhusu jambo flani. Jukwaa linaweza kuwa;
- Facebook messenger chat Bot (messenger)
- Facebook group
- Whatsapp group
- Email list
- Youtube subscriber etc
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;
PIUS J. MULIRIYE
0717375782 | WHATSAPP
0754745798 | CALL | TEXT