NJIA TANO (5) BORA ZA KUKUZA BIASHARA YAKO.

Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wafanyabiashara walio wengi ni kutokujua kiundani juu ya biashara zao. Kutokana na changamoto hiyo ya kutokujua kiundani biashara zao, wafanyabiashara hao walio wengi hujikuta biashara zao huwa haziwi za muda mrefu na hata pale zinapokuwa za muda mrefu huwa hazikui.

Naamini kwa kuwa lengo lako ni kukuza biashara, ni vyema kwa kupitia makala haya, ukafahamu pia baadhi ya mambo muhimu yatakayokusaidia kukuza hata biashara yako. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na maisha marefu na yenye kukua siku hadi siku.
 1. Ongeza maarifa kwa kujifunza.
  Kama kweli unahitaji mafanikio zaidi ya kiabiashara ni vyema ukawa ni mtu wa kujifunza kuhusiana na biashara yako. Ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wafanyabiashara wengine kufanikiwa. Kujifunza huku kukupe muda muafaka wakugundua pale ambapo wafanyabiashara wengine wanashndwa. Baada ya kujua wanashindwa wapi kwako ifanye kama fursa ya kuboresha biashara yako. Kufanya hivyo kutakufanya uongeze wateja kwani utakuwa mbunifu zaidi.
Acha kuridhika na hali uliyonayo.
 1. Badili tabia zako.
  Moja ya chachu nzuri ya kukufanya ukue kibiashara ni lazima uweze kujua vizuri tabia yako. Inawezekana wewe unajiona upo sawa ila kumbe sivyo unavyofikiri. Hata hivyo ili kuweza kujua ni ipi tabia yako ni vyema ukafanya uchunguzi ili kujua watu wanakuzungumziaje wewe? Kufanya hivyo kutasaidia kwa sababu watu wengine ndio wana picha kamili juu ya wewe na biashara kwa ujumla. Pia ili kuweza kufanikiwa ni lazima uweze kubadili tabia uliyonayo ya uvivu na ongeze juhudi za kiutendaji katika kufanya kazi.
  3. Tenga muda wa kufikiri kuhusu biashahara yako.
  Moja ya mbinu ya kuweza kukuza biashara yako ni kuweka muda kwa ajiri ya kujua biashara yako inakwenda vipi. Biashara zilizo nyingi huwa hazina maisha marefu kwa sababu wahusika hawa na muda wa kutosha kuhusu kufikiri jinsi gani biashara inakwenda bali walio wengi hutazama faida tu. Kufanya hivyo tambua biashara yako hatakuwa na Maisha marefu ni vema ukawa mzuri kujua utendaji wako wa kibiashara na changamoto zake na jinsi ya kutatua.
  4. Tambua mchango wako wa watu wengine.
  Ukitaka kufanikiwa zaidi ni vyema ukajua ni kwa jinsi unavyojenga mahusiano mazuri pamoja na wafanyabiashara wengine  na wateja wako pia. Mchango mzuri uliona nao utakufanya uongeze wateja wengine. Kwa mfano unauza biashara fulani ghafla ukaishwa bidhaa fulani harafu mteja akaja kuuliza bidhaa hiyo, usimwambia mteja huyo kwamba kama huna bidhaa hiyo mwambie ngoja nikakuchukulie kwenye stoo. Na kwa kuwa wewe huna bidhaa hiyo nenda kwa jirani yako nenda ukanunue na uje kumpa mteja huyo. Kufanya hiyo kutakufanya uweze kujenga mahusino na wafanyabiashara nyingine pia njia ya kuongeza wateja na kufanikiwa zaidi.
  5. Usiridhike na hali uliyonayo.
  Kuwa mfanyabiashara mkubwà ni lazima kuwa katika imani ambayo inatamani kufanikiwa zaidi. Maana yangu hata kama wewe unajiona tayari umefanikiwa wewe jione bado una kiu ya kufanikiwa zaidi. Kama wasemavyo kwamba pesa haitoshi basi hata wewe una deni la kufanikiwa zaidi. Moja ya kufeli kwa biashara ni pale mtu anapoona amepata mafanikio na yeye anaridhika . Kuridika ni adui wa mafanikio. Kuridhika ndiko kunako turudisha nyuma watu wengi sana. Pia nikumbushe ya kwamba kufeli sio kushindwa ni sehemu ya mafanikio.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako. 
Kama unataka kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani kama vile BATIKI, SABUNI, CHAKI, SHAMPOO n.k. kwa njia ya mtandao basi tembelea www.piuscollege.wordpress.com
Wasiliana nasi Whatsapp (only) | 0717375782


1 thought on “NJIA TANO (5) BORA ZA KUKUZA BIASHARA YAKO.”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *