Tutafakari pamoja hoja hizi za mwenzetu ole mushi

TUMEMWACHIA RUGE JUKUMU LA KUFUNDISHA WATANZANIA NINI MAANA YA FURSA?

Na Thadei Ole Mushi.



#Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

#Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

#Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

#Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha.

#John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

#Sisi tumengangania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote…..

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

#Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

#Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha. 

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye. 

#Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji. 

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga.  Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

#Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

#Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?

POST HII NILIANDIKA NOVEMBER 2017

Kikichonifanya leo nikairudia ni hii tweet ya Nh Makamba. Hapa analalamika kama raia wa kawaida kabisa kuhusiana na ubovu wa elimu yetu.

Najiuliza maswali na swali kubwa ninalojiuliza ni kwa nini mawaziri wetu, wabunge wetu ambao ni Vijana wanashindwa kuandika mswada wa kufanya marekebisho ya elimu yetu? 

Je Kulalamika tu mitandaoni kama raia wa kawaida kunasaidia nn?…. hawa ni watu ambao wanaweza kubadilisha hali ya Mambo kwa vitendo ila nao wanalalamika. 

Dah!!!!

Ole Mushi.

0712702602

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *