Jinsi ya kutumia uwoga uliokuwa nao ili kufikia mafanikio makubwa

Woga ni kitu ambacho watu wote wanacho, hakuna mtu anayeishi duniani na ikawa hakuna kitu asichokiogopa na kama yupo mtu wa aina hiyo basi atakuwa ana matatizo ya akili. Lakini kwa wenye akili, kila binadamu duniani lazima atakuwa ana kitu kinachomfanya awe na woga fulani. 

Wengi wetu huwa tunafikiria kuwa woga ni kitu kibaya, lakini ukweli ni kwamba woga si kitu kibaya, kwa kweli woga ni kitu kizuri na ni ishara ya  kuwa unatakiwa kuchukua tahadhari au kujiandaa na hilo jambo linalokutia uwoga. 
Kwa mfano kama huna kazi na umeishiwa na pesa na unatakiwa ulipie pesa ya chumba unachoishi uwoga unakuja. Hivyo unatakiwa ujiandae kwa kwenda nje kupambana na kutengeneza pesa ambayo itakuwezesha kulipa kodi ya chumba unachoishi. Huo ndio uwoga.
Lakini cha ajabu na tofauti ya watu wanaofanikiwa na watu wanaohangaika katika kupata mafanikio ni kwamba watu wenye mafanikio huwa wanajua kwamba kitu ambacho naogopa kufanya ndio natakiwa kukifanya ili kupata mafanikio. Na wale ambao hawafanikiwi huwa wanakimbia ule woga wao, yaani hawapo tayari kufanya kile wanachokiogopa. Kwa kiingereza uwoga unajulikana kama FEAR, herufi hizi zina maana ya kwamba false evidence appear real, ikiwa na maana vitu vya uongo au ushahidi wa uongo unaoonekana kama kweli.
Kwa hivyo ukiogopa kitu huwa unatengeneza picha ambayo si ya kweli. Kwa mfano kama unaogopa kuanza biashara unaweza kutengeneza picha ya kwamba nikifanya hivi watu watanicheka, au pesa yangu itazama au nitashindwa kuiendesha, vitu ambavyo havina ukweli wowote ndani yake. Watu wa saikolojia wanasema “Woga unawaumiza sana watu kuliko kufeli” yaani ni bora ukafanya kitu unachohofia kisha ukafeli kuliko kuwa hujafanya kabisa kwa sababu ya uwoga wako. Hii ni kwa sababu ukifanya kitu hata kama ukafeli lakini tayari kuna mambo utakuwa umejifunza na wakati ujao unaweza kuyakwepa yale yaliyokufelisha mara ya kwanza. Hivyo kama una jambo ambalo sasa hivi unatakiwa ulifanye lakini haulifanyi kwa sababu unaogopa.
Nakuhakikishia kama utafanya maamuzi na kuanza kulifanya hilo jambo  linaweza kukutoa katika matatizo uliyokuwa nayo sasa hivi.
 Watu wengi huwa wanapenda kuniuliza, Pius nifanye nini ili nipate mafanikio, au ni nini siri ya mafanikio?.
HAKUNA SIRI YA MAFANIKIO, Mafanikio ni kufanya tu yale mambo ambayo unatakiwa kufanya lakini unatafuta kila sababu ya kutofanya.
Mfano mzuri hivi karibuni nilitoa challenge kupitia Group la WhatsApp, kwamba kila mtu arekodi video moja inayoelezea biashara yake. Challenge hii niliitoa kwa watu zaidi ya mia tatu (300) lakini, ni mtu mmoja tu ndiye aliyenitumia video aliyorekodi. Baada ya hapo watu wanakuja tena na kuuliza Pius nifanye nini ili nipate mafanikio, jibu ni kwamba fanya kile unachoogopa kufanya utafanikiwa. Kama sasa hivi kuna kitu unaogopa kukifanya anza nacho hicho kila siku.
Nakupa challenge kwamba kila siku ukiamka andika vitu ambavyo unatakiwa uvifanye, kisha angalia ni kipi unakiogopa kati ya hivyo na uanze na hicho. Nakuhakikishia hicho kimoja unachokiogopa ukikifanya kitakupa mafanikio makubwa kuliko vingine. 
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;
Pius Justus Muliriye
0754745798

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *