Habari rafiki yangu, naamini unaendelea vyema na kuboresha maisha yako.
Leo nataka nikushirikishe kitu muhimu sana ambacho kitaweza jubadilisha mtizamo wa baadhi ya mambo ambayo ulikuwa ukiyafikiria ni kweli kumbe sio kweli.
katika dunia ya sasa kuna mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakikuwa kwa kasi ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, naamini wewe ni mmojawapo wa watumiaji wa mitandao hiyo.
Katika mitandao watu wanafanya biashara zao na zinakuwa kwa kasi kabisa na wanapata vipato vikubwa sana, na kuna wengine hawajui kama unaweza kupata kipato kikubwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Kuna wengine wamekuwa wakijua kuwa ni rahisi kupata fedha kwa kutumia mitandao na wanachokijua ni kwamba ukipost kitu chochote kile na watu waka click basi kuna kiasi cha MB zinaingia kama hela kwenye akaunti yake.
Ukweli ni kwamba, katika ulimwengu wa biashara ya mtandao hakuna kitu kama hicho na wala hakitakuja kutokea, unachotakiwa kujua ni kwamba ili upate pesa mtandaoni ni lazima ufanye kazi ya ziada ambayo mwisho wa siku itakulipa vizuri sana.
Mimi nimenufaika na matumizi ya mtandao kukuza biashara yangu na sasa nianaingiza kiasi flani kila siku, na hii imetokana na kujifunza kuhusu mtandao na kufanyia kazi.
Nikuuize swali tu, utajisikiaje unapopigiwa simu na mtu anataka akulipe kwa huduma unayotoa? au utajisikiaje unaamka asubuhi unakuta akaunti yako ya mtandaoni imeingiza kiasi flani cha fedha?
Naamini utajisikia vizuri sana.
Kaa nami na tembelea mtandao huu kila siku ili upate kujua namna sahihi ya kufanya ili uweze kuongeza kipato chako kupitia mtandaoni.
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako.
Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com