NGAZI AU LIFTI

Kwenye jengo lefu hasa Ghorofa ukiingia ndani ya jengo hilo utakuta namna mbili za kukutoa chini na kukupeleka juu au kwenye floor mojawapo katika jengo hilo.

Namna hizo mbili ni lifti au ngazi. Lifti umfikisha mtu haraka sana lakini njia ya ngazi huchosha kama unaenda mbali kwa juu. Hivyo watu wengi hupendelea kupanda lifti.

Tunaporudi kwenye mafanikio kuna Lindi kubwa la watu ambao wenyewe kwao wanapenda kupanda lifti tu. Yaani kwao hawataki kabisa kusikia kuhusu ngazi.

Lakini ukweli ni kwamba kwenye mafanikio hakuna lifti kuna ngazi tu, na lazima upande ngazi moja baada ya nyingine ndipo ufike juu.

Kuna watu wengi ambao bado wanaamini kwamba kufanikiwa ni bahati lakini sio kweli kabisa. Lazima uangaike, upambane ili kuhakikisha unafanikiwa.

Kuna maumivu mengi sana wakati wa kupanda ngazi lakini ndiyo njia nzuri sana kwenye mafanikio. Watu wanaopenda lifti mara nyingi huwa na mafanikio ya muda mfupi. Lakini wale wanaopanda ngazi moja baada ya nyingine upata mafanikio ya muda mrefu.

Usikubali na kutaka mafanikio ya muda mfupi yatakuangaisha mno rafiki yangu. Kuna watu wengi wanapenda kupata pesa za bure bila kuzifanyia jambo lolote.

Siku hizi kwenye WhatsApp utaona anakutumia eti fungua link upate dola 500?. Dola 500? Kwenye kufungua link tu?. Huo ni upotezaji wa muda tena mtu akikutumia link kama hiyo usijisumbue kuifungua.

Utakuta siku hizi vijana wengi wanapenda kubeti lakini historia inaonesha kwamba hakuna aliyewahi kufanikiwa kiuchumi kutokana na kubeti. Kwanza kubeti ni mchezo wa kupoteza (The game for losers). Ulishawahi kujiuliza unaposhinda 13000/= wanakuwa wamepoteza pesa watu wangapi? Huwa nacheka sana asubuhi unaamka unamkuta kijana ameketi kinyonge utafikiri kafiwa ukimuuliza kulikoni atakwambia “Mkeka umechanika.” Kwanini umeamua kujibebesha stress za bure ukiwa kijana. Hujui kwamba stress zinaua watu taratibu?

Usipende lifti, mafanikio yanahitaji watu wanaopanda ngazi. Leo hii anza na kusema nitaanza kupanda ngazi na nimeacha Lifti maana hainipeleki popote.

Nakutakia wiki njema.

Mafanikio yako yako mikononi mwako.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *