Unapotaka kuuza bidhaa yako usimweleze mtu kwa namna ya bado unaumiliki wa bidhaa uliyokuwa nayo ila mweleze mtu katika hali ya kujiona ni mmiliki wa kitu unachouza.Hakuna mtu anayependa kununuliwa lakini kila mmoja anapenda kuwa mmiliki.
KWANINI MAUZO YAKO SIO MAZURI?
Hili ni swali ambalo kila mmoja anajiuliza katika biashara yake. Hakuna mjasiriamali wala mfanyabiashara ambaye anaweza kunufaika na shughuli yoyote bila kuuza.Napoongelea kuhusu kununua umiliki na kuweza kuwa na maamuzi juu ya kitu flani.Nikwambie kitu kimoja kwamba kila mmoja anauza haijalishi unabiashara au huna biashara lakini lazima uwe na kitu ambacho unauza yanaweza kuwa maneno yako au matendo yako. Nakwambia hivi kwasababu kabla ya mtu kuchukua bidhaa yoyote kwako kwanza kabisa lazima maneno yako yaweze kununua fikra zake kabla yeye kununua bidhaa yako kwa hela yake ndio maana biashara nzuri ipo kwenye kujenge mahusiano na wateja wako,hapo ndipo biashara ilipo na sio pengine. Usiangalie hela unayoipokea sasahivi kutoka kwa mteja wako tuu lakini angalia kujenga mahusiano mazuri na mteja wako ili upate hela nyingi kutoka kwake kwa baadae. Ukiangalia watu wengi kwenye biashara wamesahau hili wao ilimradi mtu kaja na kuondoka basi.
Ngoja leo nikupe siri moja kwa ufupi haswa kwa wateja ambao unawahudumia kwasababu watu wengi hukosa kufanya mauzo mazuri kwa kutokujali kujenga mahusiano mazuri na wateja wao katika biashara zao. Katika makala zangu za kipindi cha nyuma nilishawahi kusena kwamba mteja wako mmoja amekubebea wateja wengine zaidi ya 30-50 usiowajua lakini hawa thelathini utawapata kwa kujenga mahusiano mazuri kwasababu zifuatazo
1. Mteja wa kwanza unayemuhudumia unaweza kuwa unamjua au yeye anaweza kuwa anakujua.
2. Mteja wako anawatu wengine ambao anawajua lakini wewe huwajui na ukijenga nae mahusiano mazuri ataweza kukuonganisha na wale usiowajua.
3. Wale mteja wako anaowajua ambao wewe huwajui na wenyewe wanawatu ambao mteja wako wa kwanza hawajui na wewe huwajui lakini mahusiano yako mazuri yanaweza kufanya kuwajua wote.
Ukiangalia kwa ukaribu biashara nzuri na ambayo itakufanya kufika mbali ni ile ambayo inajenga mahusiano mazuri na wateja wake.Usiridhike kuona watu wanaondoka na wala hufanyi chochote cha kuwafanya kurudi tena haswa kujenga nao mahusiano mazuri.
Tafadhari naomba ujisajiri hapa chini ili uwe unapokea ofa zetu mbalimbali zinapokuwa hewani.
Ni mimi mpenda maendeleo yako
PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
0657128567