JINSI YA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WATEJA WAKO

Mahusiano mazuri na wateja wako huwepo kwa kutambua tabia zao.Lakini imekuwa ngumu sana kwa watu kujenga mahusiano haya kwasababu watu kuwa wavivu wa kufanyia kazi upande huu,wengi wanadhani kuwa na bidhaa au huduma tu tayari ni biashara ambayo itakutoa kimaisha,kumbuka mahusiano mazuri na wateja wako baada ya kuwa na biashara ndiyo biashara yenyewe yenye mafanikio.Kuna mtu anajisemesha “ya nini kujenga mahusiano na huyu mteja wakati ameshanipa hela yake?” haya ni maneno ya mfanyabiashara ambaye hana malengo na biashara yake na wala hana maarifa kuhusu biashara.Katika kitabu cha Akili Ya Ushindi ambacho kitatoka mwe, unaokuja mwishoni nimesema Mtu ambaye kila siku anafanya manunuzi ya 2000 kwa mwaka atakuwa amekuchangia 730,000/= chukulia kwa wiki mtu anafanya manunuzi ya 20,000/= katika biashara yako kwa mwaka atakuwa amekuchangia 960,000/= hapa nakupigia hesabu kwa mtu mmoja tuu,sasa chukulia haujajenga mahusiano mazuri na watu hawa unadhani viwango hivi utavipata? HAPANA hutavipata.

Leo nikupe njia za kujenga mahusiano ili hivi viwango vya pesa visikupite pamoja na kujenga jina la biashara yako.

1. Tafuta lugha nzuri ya kutengeneza urafiki baina yako na mteja wako.Usipende kuwa mkimya sana zungumza na mteja wako,mchangamkie.

2.Toa ofa kwa wateja wako haswa wale ambao huwa wanakuja kuchukua huduma kwako ikiwezekana hata na wale ambao wanakuja mara mojamoja kwako.Inaweza ikawa punguzo la bei kwenye huduma flani au kwenye bidhaa flani.

3. Tenga muda wa kusabahi watu walioko karibu nawe kama unatumia mitandao pia unaweza kutenga muda wa kuweza kuwasiliana na wateja wako wa mbali kwanza watatambua uwepo wako na wataona jinsi unavyowathamini.Najua sio wateja wote ambao unaweza kuwafanyia hivi lakini kwa wateja baadhi inatosha.

4. Usitumie nafasi ya kujitambulisha kwa watu kwa kujificha,weka wazi unachokifanya watu wajue haswa kwenye mikutano,au sherehe ukipata nafasi ya kujitambulisha hapo ni sawa na kuletewa wateja anza na wewe ni nani,unafanya nini,ofisi yako ipo wapi, toa mawasiliano,na hakikisha unawakaribisha.

5.Nenda na wakati tumia mitandao ya kijamii kuunganika na watu siku hizi mitandao ya kijamii inaweza hata kuwa kama business card yako mfano kwangu mimi business card yangu ni mtandao wa linkedln wako ni upi?

6. Kuwa msafi na vaa nguo za heshima.
Hii sitaielezea sana ila tambua usafi wako na mavazi yako kwanza huleta tafsiri ya tabia yako na wateja wengi wa kudumu hupenda kujenga mahusiano na mtu wa namna hii.

Ulikuwa nami:

Pius Justus
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

1 thought on “JINSI YA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WATEJA WAKO”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *