Tangu nimalize kidato cha sita kuna kitu kimoja kimekuwa kikinisumbua sana ndani ya kichwa changu bila ya kupata majibu.
Kitu chenyewe ni “Nini siri ya Mafanikio“?
Kwa nini akina Bill Gates, Said Salim Bakhressa na Mo Dewji wafike walipo fika na kupata mafanikio makubwa na sisi wengine tuhangaike?
Je wao wana akili kuliko sisi?
Wamezaliwa katika familia ya kitajiri?
Au wana bahati?
Japokuwa kuna majibu tofauti ya siri ya mafanikio yao kuna sifa kuu mbili wote wanayo.
Sifa ambazo hata sisi tunaweza kuiga kwani sifa hizo hazihitaji hela.
Nimegundua sifa hizo baada ya kusoma ma mia ya vitabu, kuhudhuria semina tofauti ndani ya nchi na kuangalia mahojiano waliyofanyiwa watu wenye mafanikio.
Sifa zenyewe ni…
- Jua EXACTLY unataka kitu gani
- Fanya kazi kama punda upate unachokitaka
Mambo hayo mawili makuu (japokuwa yapo mengine) ndio tofauti ya Bakhressa na kijana aliyechoka nyumbani.
1: Jua unataka nini:
Rafiki yangu mmoja alibahatika kuonana na Said S. Bakhressa na kumhoji maswali kuhusu maisha yake na mafanikio.
Moja ya swali aliyemuuliza ni,
“Umefanya nini kuhakikisha umepata mafanikio uliyokuwa nayo“.
Bakhressa akamjibu,
“Mimi siku zote nilikuwa nikijiuliza swali, ‘nifanye biashara gani ambayo itanifanya kila mtanzania aweze kunilipa Tshs. 1000 kila siku?’
Baada ya hapo nikwa ninatafuta bidhaa rahisi zenye kuwanufaisha watanzania na hatimayi kuwafanya wengi wao kuweza kunilipa Tshs. 1000 kwa siku.“
Na ndio maana mifumo ya biashara ya Bakhressa ni yale ambayo bidhaa zake rahisi na kuwalenga umati mkubwa watu.
Bakhressa alijua exactly anataka nini.
Bill Gates alikuwa anataka kila nyumba marekani iwe na computer na kazi yake ilikuwa kutengeneza operating system (mfumo wa kuendesha kompyuta) yenye kurahisisha utumiaje wa kompyuta kwa watu jambo ambalo liliwavutia watu wengi kununua kompyuta.
Bila ya Windows mawasiliano yangu na yako sasa hivi ingekuwa ngumu.
Je wewe unajua unataka nini?
2: Fanya kazi kama Punda:
Kuna msemo unasema,
“There’s NO substitue for hardwork“
yaani…
“Hakuna mbadala wa kazi nzito“
Na Ralph Edwardo Emerson alisema,
“Genius is 1% inspiration and 99% perspiration“
yaani…
“Uwerevu ni 1% ya mawazo mazuri na 99% kupumua.“
Hakuna short cut ya kuchapa kazi.
Kama utaweza kujijengea tabia ya kufanya
- kazi ya siku kwa masaa,
- kazi ya mwezi kwa wiki na
- kazi ya mwaka ndani ya mwezi mmoja
Uvivu hauna nafasi kwa watu wenye mafanikio.
Kama umezoea kulala kwenye kochi na kuangalia Mpira na Game of Thrones na unalalamika maisha magumu, basi unahitaji kufanya mabadiliko ya haraka.
Jipatie kitabu kizuri sana cha FACEBOOK MASOKO kinachofundisha namna ya kufanya biashara kwa kutumia mitandao ya kijamii hasa facebook kunasa wateja wengi.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,