ACHANA NA WAJUAJI TEMBEA NA WAFANYAJI


Achana Na Wajuaji Tembea Na Wafanyaji













Mjuaji ni mtu anayejifanya kujua kila jambo. Mara nyingi  ukikutana naye atakwambia jambo hili alifanywi hivi linafanywa hivi au acha kufanya hivi fanya namna hii.

   Wafanyaji ni wale watu wanaofanya mambo yanayoonekana, hawa si wababaishaji.

Mara  nyingi ukiwa unafanya kitu ambacho unaamini ni ndoto yako wajuaji watakao kujia ni wengi. Watakuja wakikwambia fanya hivi, lakini wao hawajawahi hata kufanya kile unachokifanya au watakuja wakisema, huwa wanafanya hivi na hawafanyi vile lakini ukiwauliza swali dogo tu kama hili “ Umewahi kufanya kitu kama hiki?” utaona wanaanza kupepesa maneno, wakisema mara ohoh niliwahi kuona mahali au huwaa wanafanya hivi. Ukiona au kukutana na watu wa namna hii ttambua hawakufahi, waepuke kama ukoma tena sio wa kukaa karibu nao.

Anza kutembea na wafanyaji. Tafuta marafiki wanaofanya kitu kama wewe unachokifanys. Tafuta watu waliowahi kufanya kitu unachokifanya maana wanajua changamoto ambazo wanakumbana nazo na jinsi ya kuzitatua.

Wafanyaji ni kama wachezaji na wajuaji ni kama mashabiki, mashabiki mara nyingi ujifanya wakijua mpira Zaidi ya wachezaji wenyewe wanaokuwa uwanjani. Kuna msemo unasema, “Utamu wa ngoma anaujua mchezaji na si mkaaji.” Mtu aliyekaa chini hawezi kuelezea ngoma ilivyokolea kama yule anayeicheza. Hapa tunaweza kumfananisha mkaaji kama mjuaji na yule anayecheza ngoma kama
mfanyaji.

Kumbe tuachane na kuandamana na wajuaji tuanze kutembea na wafanyaji, kama ni biashara tafuta mawazo na ushauri kwa watu wanaofanya biashara kama yako au tafuta watu wenye ufahamu kuhusu biashara husika. Kama ni masomo  tafuta mtu aliyesoma masomo husika au mwenye ujuzi wa masomo husika, ndiyo maana hata kidato cha tano na sita mwanafunzi wa masomo ya Sanaa anafundishwa na mwalimu wa masomo ya Sanaa, na mwanafunzi wa sayansi anafundishwa na mwalimu wa sayansi. Huwezi kuugua na kwenda kwa injinia akuandikie dawa ya kutumia, lazima uende kwa daktari ndiye atakuandikia dawa sahihi. Lakini ukitaka ushauri kuhusu nyumba yako lazima uende kwa injinia huwezi kwenda kwa daktari.

Wasikilize wafanyaji usiwasikilize wajuaji. Achana na wajuaji, tembea na wafanyaji.

“Mafanikio Yapo Mikononi Mwako.”

Jipatie kitabu hiki kitakachobadili maisha yako kabisa, utajifunza namna mbalimbali za kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani na utengeneze faida mara dufu. Ni muda wa wewe kijana kuanzisha kiwanda chako nyumbani kwako na ufikie malengo yako. unaweza kukipata kwa kubonyeza picha hii; 


















Asante;
Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *