KIPAJI NDIO UTAJIRI WAKO


Kujitambua ni Hatua ya kwanza kuelekea kwenye Mafanikio.

Kujitambua wewe ni nani ni hatua ya kwanza kwako kuanza kufanya mambo makubwa na kutimiza ndoto zako.
Watu wengi wanashindwa kujitambua wao ni nani hivyo wanaishia njia bila hata kujua uwezo walio nao. Kama hujajua wewe ni nani huwezi kujua uwezo wako ukoje.
Embu jiulize simba mkubwa ambaye hajitambui yeye ni simba hawezi kuwinda. Hawezi kutambua pia nguvu alizonazo.
Mfano mzuri kwa wanyama tunaoweza kuwatolea mfano ni tembo. Tembo ni mnyama mkubwa sana ambaye pia ana nguvu kubwa mno. Lakini kitu cha ajabu analiwa na mnyama mdogo sana Simba, sio kwamba tembo hawezi kupambana na simba na akamshinda anaweza lakini tatizo lipo kwenye kujitambua.
Akijitambua yeye ni nani ataweza kujua pia na uwezo alio nao.
Kwenye jamii zetu tuna watu wengi sana wenye uwezo mkubwa, nguvu nyingi za kutimiza ndoto zao, lakini wanashindwa kufanya chochote kwa kua tu hawajitambui. Ili uwezo kufikia chochote kwenye maisha yako ni lazima ujitambue kwanza wewe ni nani na una uwezo gani. Najua unatambua jinsia yako lakini kutambua jinsia tu haitoshi unakua kama tembo mkubwa mwenye nguvu lakini hawezi na hajui kuzitumia.
“To understand yourself is the first step of achieving your dreams and make them reality.”
Kama hujajitambua wewe ni mwandishi bora sana huwezi kuanza kuandika na kufikia mafanikio makubwa. Kujitambua ni hatua ya kwanza kuelekea mafanikio.
Leo ni wakati wako wa kukaa chini na kutafakari wewe ni nani na una uwezo gani ndani yako. Una vipaji vya kipekee sana ndani yako ambavyo hakuna mwingine mwenye navyo, kuvitambua hivi kunakupeleka kwenye njia ya mafanikio makubwa sana.
Hatua za Kujitambua.
Tenga muda ukiwa peke yako.
Tenga muda ambao utakua mwenyewe na uanze kutafakari maisha yako na ni kwanini upo duniani. Hapa unaweza kua na angalau masaa matatu ukiwa na kitabu chako na kalamu. Kaa chini na uanze kuandika vile vitu unavyopenda kuvifanya kuliko vingine. Andika uwezo wako ulio nao juu ya vitu hivyo. Jiulize unawezaje kuvitumia vitu hivyo ndani yako ili ufikie mafanikio.
Vitu vyote unavyoviona duniani ubunifu wa kila namna na mambo mengi mazuri sana yametoka ndani ya watu. Hivyo ni kwamba hata wewe unavyo vitu vya kipekee sana vya kuacha hapa duniani.
Anza kujitambua wewe ni nani na utaweza kufanya mambo makubwa sana duniani na kulitimiza kusudi lako.
Kila siku kua na muda wako peke yako angalau nusu saa ambapo utakua unatafakari una nini ndani yako na unawezaje kuacha hapa duniani. Usikubali kurudi na vitu vya pekee sana ulivyozaliwa navyo. Ulipewa vitu hivyo ili uvitoe kwenye dunia hii. Vitu hivyo ndio vitakufanya wewe upate furaha na chochote kile unachokitaka iwe ni magari, nyumba nzuri, mke au mume anaendana na kusudi lako pamoja na vingine unavyovitaka.
Nikwambie hujachelewa bado una nafasi ya kufanya mambo makuu sana na dunia ikatambua uwepo wako. Wewe ni mtu wa pekee sana sijawahi kuona. Ila tu nibado hujajitambua. Milango itaanza kufunguka pale utakapozitambua zawadi zilizopo ndani yako. Utaacha kufanya kazi tu ili upate pesa na utafanya kile kinaleta furaha ndani ya moyo wako maana hicho ndio kina utajiri wote.  Hujachelewa unaweza kuanza leo haijalishi una miaka mingapi sasa. Bado unaweza kuimba ule wimbo wa kipekee ndani yako na watu wakausikiliza.
Kama unapitia changamoto yeyote ya maisha, hujajitambua wewe ni nani, hujatambua kusudi lako, hujatambua uwezo wako na vipaji vilivyoko ndani yako tafadhali wasiliana nami hapo kwa msaada Zaidi. Hamu yangu ni kuona unafanikiwa na ni ngumu sana wewe kufanikiwa nje ya kusudi lako. Kama uwezo wako mkubwa upo kwenye kuimba ukienda kucheza mpira huwezi kufikia mafanikio makubwa na itakuchukua muda mrefu sana kufanikiwa. Anza leo kuliishi kusudi lako.
Imeandaliwa na
Jacob Mushi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *