Kwa miaka ya hivi karibuni Watanzania wengi sana wanajishughulisha sana na UJASIRIAMALI. Safi sana, hvyo kila mjasiriamali anahitaji Masoko.Masoko ni Matokeo ya Mahusihano kati yako na mteja.
Soko halitoki hewani ni mchakato.Kitu cha msingi kabisa katika KUJENGA SOKO LA BIDHAA YAKO NI kutengeneza lugha ya soko. Watu wa kiswahili wanahta Rejesta ya soko au watoto wa mjini wanahita swaga za soko.
Mfano SOKO lako ni yule mteja wako au mtumiaji wa bidhaa yako. Siyo mpaka uwe kariakoo au Buguruni ndo ujue uko sokoni.Sokoni ni pale anapopatikana mtumiaji wa bidhaa yako hivyo ukiwa mahali alipo jenga lugha nzuri ya soko.
Lugha ya masoko au soko ni lugha ya mahusihano kati yako na mteja inayowawezesha kufanya biashara.Wengine wanaita lugha ya Biashara.Wajasiriamali wengi wanapenda kufanya biashara ila hawana lugha ya biashara au Masoko.Sasa kama huwezi kuongea vizuri na soko lako utamuuziaa nani?
LUGHA YA MASOKO ndio muhimili wa biashara au mauzo. Unaweza ukawa na bidhaa au huduma nzuri ila kwa kukosa lugha ya soko ukawa hupati wateja. Yaan unaongea lugha tofauti na ya mteja.
Kama mjasiriamali jitahdi sana kujenga lugha ya soko ili uwezeckupata soko kubwa kabisa.Tunakosa masoko kwa kuwa na lugha isiyoendana na soko.
JINSI YA KUJENGA LUGHA YA SOKO
- Jenga tabia ya kumkaribisha mteja kwa sura ya tabasamu.Hii itamfanya mteja kujiona yeye wa thamani kumbe wewe unataka hela yake.
- Kuwa na bei inayovutia, wengi wanataka kupata faida kubwaa ili Hali soko lao ni LA watu wa kawaida. Panga bei inayofiti soko lako. Kwa nini wachina wameteka soko letu. Wanaongea na sisi kupitia beiAcha bei yako iongee kuliko maneno yake
- Usishindane na mteja Bali kubali anachokueleza na ahidi kuufanyia kazi ushauli wake.
- Kamwe usimpinge mteja wako Bali msikilize asemacho. Wajasiriamali wengi hawapendi kukosolewa wawapo sokoni.Hii inamfanya mteja kujiona ni rafiki kwako pale anapokupa ushauri ukauchukua
- Shukrani.Mshukuru mteja hata kama hajanua Bali kwa shukurani yako kutamfanya aje anunue siku nyingine
Huwa nawauliza watu Leo hii mi Nauza Mende na soko linabaki inakuwaje we we unakosa kuuza mboga mboga au nyanya zako Hapana shugulikia eneo LA lugha.
Mimi ukinipa bidhaa yoyote siwezi kosa kuuza kozi kila siku najinoa katika eneo LA lugha.Mfano anaweza akaja mteja ambaye sijawah muona lakini nikimpokea anaweza hisi namjua au tunafahamihana naye kitambo.Hapo napitishia vimaneno vya mzaa au story Fulani inayoendana na yeye .Hii ni kumteka kisaikolojia ajue na kujenga urafiki naye ili asiponunua Leo basis anitafute Sikh nyingine.
Pia anaweza akaja mteja nikamteka hvi kaka au Dada kama nimekufananisha hivi anyware karibu sana hii ni bidhaa Fulani Fulani. So wakati nishamchanganya na yeye kuanza kufikiria kama ananijua mimi naanza kumpiga shule ya bidhaa au huduma yangu.
SIKU ZOTE JIFUNZE KUMMILIKI MTEJA KWANI YEYE AKIKUMILIKI hapo huuzi maana atajua we mbabaishaji.Pia weza kuimudu kuielezea bidhaa yako. Kama unauza bidhaa ila huna majibu ya maswali ya mteja hapo hakuna biashara.Mteja anauliza yawezekana anaijua bidhaa kuliko wewe.Ila wewe tumia point chache tu kumudu.
NIWEKE WAZI CHANGAMOTO KUBWA AU SABABU KUBWA YA WAJASIRIAMALI KUKOSA MASOKO NI KUTOKANA NA KUKOSA UJUZI WA LUGHA YA MASOKO.
Waliojijengea lugha ya Masoko wanapiga pesa hata kwa vitu vya ovyo.Nakwambia Leo mimi Nina oda ya MENDE si mchezo wapo wanaotaka mbegu, wengine unga na wengine cage za mende.Ila kuna MTU anashamba LA MATIKITI Mkuranga ana haha na wateja.
Ndugu zangu wajasiriamali BORESHENI lugha iwe ya masoko Ili uweze faidi au jipatia MASOKO mengi na makubwa.MASOKO Yanaanza na wewe Amuua sasa ujizolee masoko.