MAMBO MATANO WANAYOYAFANYA WATU WALIOFANIKIWA KILA SIKU (FIVE THINGS SUCCESSFUL PEOPLE DO EVERY DAY)

Habari mdau wa maendeleo, natumai u mzima wa afya ya kutosha, ni jambo la kumshukuru Mungu kwa neema hiyo, na kama hautakuwa salama basi usijali ni changamoto za maisha tu, hayo ni mapito na kila kitu kitakuwa sawa tu.

Leo ninapenda nikushirikishe mambo matano (5) muhimu katika maisha ambayo kila aliyefanikiwa katika Nyanja ya maisha yoyote anayafanya kila siku. Natumaini ukifata haya mambo nawe pia utakuwa miongoni mwa waliofanikiwa.
  • Kitu cha kwanza baada ya kuamka asubuhi ni kumshukuru Mungu.
Asikudanganye mtu, kila siku asubuhi watu wote waliofanikiwa hawaachi kumshukuru Mungu, haijalishi unaabudu kitu gani, lakini lazima upige goti na kusema Asante Mungu kwa kuiona siku nyingine tena.
  • Fanya mazoezi ya viungo.
Watu waliofanikiwa siku zote baada ya  kuamka huwa wanafanya mazoezi ya viungo ili kuweka mwili sawa, hii husaidia ubongo kuamka na kuwa fiti kupokea mambo mapya siku hiyo, pia mazoezi huondoa uchovu wa mwili.
Ukitaka kufanikiwa katika siku yako, ni lazima ufanye mazoezi ili mwili wako uwe stable na uwe  tayari kupokea vitu vipya, vinginevyo siku yako itaisha ukiwa kama mgonjwa. 
  • Kula kifungua kinywa  chenya Afya.
           
Hapa watu wengi huwa wanachemka kwa sababu hatufati utaratibu wa kula kifungua kinywa chenye afya. Hapa hatumaanishi kula wali maharage na chai, hapana, hapa tumaanisha kula matunda, au juice, mbogamboga na vitu vingine natural ili kuweka mwili wako wenye afya ya mwili na ya akili.
  • Safisha inbox yako kila siku
Hii ina maana sana katika mafanikio, hii inakuwezesha kuangalia meseji ambazo hujafanyia kazi na kuzifanyia kazi, hii itakufanya uianze siku ukiwa huna kitu kitakachokusumbua siku hiyo.
  • Andaa mpangilio wa siku yako hiyo.
    Hii kwa kiingereza inaitwa TO DO LIST, hii itakusaidia kujua siku yako itaendaje, hii ni muhimu sana kwa sababu siku yako utakuwa umeipangilia vizuri na itaisha ukiwa huna majuto yoyote ya kupoteza muda.
    Hayo ndio mambo matano ambayo kila aliyefanikiwa hufanya kila siku, jaribu pia na wewe uone mabadiliko katika maisha yako.
    Nikutakie kila lakheri katika utekelezaji wa haya.
    Tafadhari share na marafiki zako kwa kubonyeza kitufe cha social network hapa chini,  facebook,  twitter au whatsapp. 
    Nikutakue kila lakheri katika kuboresha maisha yako. 
    Pius Muliriye Justus 
    0754745798
    0657128567
    piusjustus28@gmail.com   

    Leave a Comment

    Your email address will not be published. Required fields are marked *