EIMU NA UHALISIA WA MAISHA

Profesa wa Chuo kikuu cha Makelele nchini Uganda, aliwambia wanafunzi kuwa:
Mafanikio ya kielimu hayana uhalisi katika maisha. Niliyasema haya:

Kuwa mtu wa kwanza darasani kwako hakuamanishi wewe utafanikiwa kimaisha.

Unaweza kumaliza chuo kama mtaalamu wa fedha au uwekezaji na haiamanishi kwamba wewe utapata au utakuwa fedha nyingi kuliko wengine. Mwanafunzi mwenye ufaulu na shahada ya hali ya juu katika kitivo cha sheria haiamanishi kwamba ndio atakuwa mwanasheria bora.

Ukweli ni kuwa maisha yanahitaji zaidi ya kuelewa nadharia ya masomo, kuyakumbuka na kuyaandika tena kwenye mitihani. Shule zinawazawadia wanafunzi kwa uwezo wao wa kukumbuka. Maisha yanawazawadia watu kwa uwezo wa kiuvumbuzi na ubunifu. Shule zinawazawadia watu kwa uwezo wao wa kuwa waangalifu, maisha yanawazawadia watu kwa uwezo wa kuthubu ka maarifa.
Shule zinawasifia wale wanaoishi kwa kufuata kanuni na sheria. Maisha yanawasifia wale wanaovunja sheria na kanuni zilizotengenezwa katika mtazamo wa kujikwamua kwa vipato halali.

*Kwahiyo naamanisha watu wasisome kwa bidii shule?*

*Lahasha, hapana siamanishi hivyo unatakiwa kusoma kwa bidii*. Lakini usiache kila kitu kikakupita kwasababu ya kupata daraja la kwanza la ufaulu.Usijiwekee mipaka darasani tu. *Pia fanya vitu kwa vitendo vya kimaisha kutokana na elimu yako*
Pata nafasi ya Kiungozi. Anzisha biashara na ushindwe.Hili ni somo zuri la biashara la 101.Jiunge au anzisha klabu. Jaribu kugombea nafasi ya Kisiasa ili ushindwe. Itakufundisha kitu katika somo la Siasa 101 ambalo usingejigunza.Hudhuria mijadala na mafunzo. Soma vitabu nje ya mtaala wa masomo yako. Nenda katika safari na shinda katika kupata ya nje….Fanya kitu unachoamini. Fikiria zaidi kuwa mtu bora na sio kuwa mwanafunzi bora.

Usifanya darasa kuwa dunia yako bali dunia kuwa darasa lako. Nenda mbele, Jaribu siasa, Jaribu kilimo,Jaribu biashara, Jaribu na kitu kingine.
Na Mungu atakujalia

*Umeipenda?*
 tafadhali watumie na wengine wajifunze.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *