HII NDIO NGUVU YA BIASHARA YA MTANDAO.

Habari rafiki yangu na msomaji wa mtandao huu wa shule Tanzania, naamini unaendelea vyema kabisa na kazi zako ili kuboresha maisha yako.Naamini umekuwa mfatiliaji mzuri sana makala zangu mbalimbali ambazo umekuwa ukizisoma kupitia mitandao yangu tofautitofauti hasa facebook na blog hii.

Leo nataka kukupa ukweli juu ya biashata ya mtandao. Inawezekana unaijua lakini hili nalokwambia linaweza kubadili mtizamo wako na kuamua kuchangamkia fursa hii.

Kuna aina nyingi sana za biashara ya mtandao, hivi karibuni biashara za aina hii zimeshamiri sana kiasi cha kuchukua akili za watanzania wengi sana na wengi wao wamekuwa wakilizwa na system za biashara hizi na wengine wamekuwa wakikata tamaa na kushindwa kufikia malengo yao.

Nyingi ya biashara hizi ni zile za kujiunga kwa kiasi flani cha fedha na kuanza kuuza products au bidhaa za kampuni flani, wengi wamekuwa wakihangaka sana na hatimaye kushindwa biashara hizo kwa kutojua namna sahihi ya kuuza na kutangaza biadhaa hizo.

Leo hii sitagusia kabisa aina hii ya biashara. Hii ni aina za biashara ambazo hata mimi binafsi zilishawahi kunipotezea muda kwa kutokujua historia na ukweli juu ya hizi biashara, na hapo ndipo nilipopata akili ya kuanza kusoma sana juu ya biashara ya mtandao kwa namna nyingine kabisa. 

Biashara ya mtandao ambayo ninakushirikisha mimi ni ile ambayo utahusika moja kwa moja wewe na kutengeneza bidhaa yako utakayoiuza mtandaoni. Najua utaanza visingizio kuwa sina biashara yoyote nitauza nini sasa mtandaoni?

Kuna aina nyingi za biashara na zote inawezekana kuziuza mtandaoni kwa urahisi kuliko unavyofikiria.

Biashara nayozungumzia ni ile ya DIGITALI (DIGITAL PRODUCTS) hii ni bidhaa ambayo kila mtu anaweza kutengeneza na kuuza mtandaoni. Najua swali lako kubwa litakuwa nitatengenezaje bidhaa hii na mimi sijui maswala ya mtandao?

Kama una swali kama hilo basi usijali, nitakwenda kukufundisha hatua kwa hatua kama utaendelea kufatilia makala zangu kila siku.

Kabla sijaingia kabisa kwenye biashara hiyo, nataka nikuonyeshe ni namna gani dunia imebadilika lakini bado wewe hujabadilika kabisa. Lengo langu ni kutaka vijana wenzangu tutengeneze pesa nyingi ili tufikie ndoto zetu mapema sana huku tukiwa tumelala na acount zetu zikiendelea kuingia pesa bila ya kufanya kazi ngumu sana kwa muda mrefu. 

muda unaoutumia kuzulula na kufanya mambo mengine ambayo siyo ya muhimu kwako nataka uutumie kutengeneza bidhaa moja ambayo itakuingizia pesa maisha yako yote huku ukiwa umelala, au ukiwa unafanya mambo yako mengine huku biashara yako inaendelea tu na acount yako inaingiza pesa tu, na hiyo ndiyo nguvu ya MTANDAO.

Vijana sana ni muda wa kutumia facebook, instagram na mitandao mingine kutengeneza pesa na si kuangalia umbea na kupoteza muda tu.

Picha hii chini ni moja ya screenshot ya acount yangu wakati nimemaliza kusoma kozi yangu juu ya biashara  ya mtandao na nikafanikiwa kuanzisha DIGITAL PRODUCT na nilivofanikiwa kuiweka mtandaoni na kuendelea na mambo yangu, usiku kucha biashara yangu ikawa inaendelea na watu wakaweza kununua bidhaa yangu bila ya mimi kuhusika moja kwa moja, ni system niliyoiweka ndio iliyonisaidia kufanya kazi badala yangu!! nina imani hiyo imekushangaza!
 na hiki ndio kiasi nilichotengeneza siku ya kwanza tu na hakuna aliyekuwa akinijua lakini niliuza huku nimelala.
Hiyo ndio aina ya biashara kila mtu hasa wewe kijana unayetafuta maisha na kufanikiwa kwa haraka lakini kwa kufanya kazi unayoipenda na kuibadili na kuiweka mtandaoni.

Hivi karibuni nitatoa video ikifundisha namna ya kubadili baishara yako au wazo la biashara yako kwenda katika mfumo wa digitali na kutengeneza pesa.

Una bahati sana wewe kijana umepata mtu wa kukushika mkono, mimi nilijifunza haya mambo kwa muda wa miaka 9 sasa tangu niko chuoni na nimekuja kuanza kuingiza pesa baada ya kuumia kwa muda mrefu na kutumia pesa nyingi nikijaribu kujifunza mambo haya. Tumia fursa hii kujifunza.

kama umesoma makala hii na umevutiwa na wazo hili na unapenda na wewe kutengeneza pesa kwa kuuza bidhaa mtandaoni kama mimi basi niandikie whatsapp 0754745798 kwamba unahitaji kujua zaidi. nitafurahi sana kupata meseji yako na tutakwenda pamoja.

asante kwa kuwa nami mpaka hapa.

Ni mimi mpenda mafanikio yako

Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

1 thought on “HII NDIO NGUVU YA BIASHARA YA MTANDAO.”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *