Habari rafiki;
Naamini umeshawahi kujisemesha mwenyewe kwamba utafanya kitu flani baadae au kesho au wiki ijayo na mwisho wake hicho kitu hakifanyiki tena na kusahaulika kabisa.
Wakati nimeanza tabia ya kusoma vitabu vya ziada mwaka 2008 nilikutana na sentensi moja ambayo ilinifanya nibadili fikra na jinsi ya kuona mambo katika mtazamo mwingine kabisa ambao ni chanya. Brian Tracy katika kitabu chake cha CHANGE YOUR THINKING CHANGE YOUR LIFE aliandika kwamba ili mtu aweze kufikia malengo yake ni lazima awe tofauti na mitazamo ya watu wengine.
Unaweza kulalamika sana sehemu ulipo haina huduma ya maji, ukongea sana na kwenye vikao ukawa ni mmoja wa watu wanaotuhumu serikali juu ya kutowajibika kwake na ukawa miongoni mwa wanaohamasisha watu kufanya maandamano kushinikiza serikali kufanya hivyo na hatimaye kupigwa na polisi na hali ikaendelea kuwa vilevile miaka nenda rudi, ukasahau kabisa kama hiyo ni fursa kwako kama mtu unayetaka kufanikiwa katika maisha. (Yaangalie matatizo katika jamii yako uifanye kuwa fursa kwako), licha ya kupata pesa utakuwa unewasaidia watu kutatua tatizo la maji.
Ukisoma kitabu cha CASHFLOW QUADRANT cha ROBERY KIYOSAKI anazungumzia watu wawili waliona fursa katika jamii ya ukosefu wa maji ambapo mmoja aliamua kuchota maji kwa ndoo na kujaza kisima na watu kuja kununua maji pale ambapo ilikuwa ni njia iliyompatia pesa lakini haikuwa endelevu kwani mtu yule akiugua siku hiyo kijiji kinakosa maji, lakini mwenzake alipotea mwaka mzima na yule wa kwanza akajua tayari fursa ile ilikuwa yake tu na amepata nafasi ya kufanya biashara, baada ya mwaka yule mwingine akarudi akiwa na mipango thabiti ya kutatua tatizo la maji na huku akitengeneza pesa huku amelala.
Alikuja na mpango wa kuchimba mifereji na kulaza bomba kutoka ziwani mpaka kijijini kwa kusaidiana na wahisani alioingia nao mkataba na hatimaye kwa siku koja kumshinda yule mwenzake aliyekuwa akichota maji kwa ndoo na kujaza kisima cha kijiji na hatimaye cashflow yake ikawa endelevu kuliko mwenzake.
Hivyo ndivyo inavyotakiwa kufikiria zaidi ya wenzako ili ufikie pale unapopahitaji.
Hujachelewa, chukua muda na kaa chini ufikirie nini cha kufanya kulingana na sehemu ulipo, usikimbilie mjini ukadhani huko ndiko kuna fursa kumbe unaziacha kijijini.
Wenzako kama wanalima kwa mkono, tafuta namna ya kulima kwa trekta, wenzako kama wanalima bila mbolea, wewe weka mbolea, wenzako kama wanategemea mvua wewe chimba kisima na umwagilie mazao yako majira yote ya mwaka, nakuhakikishia utafikia malengo yako.
Wakati nimemaliza mafunzo yangu katika shirika la kiserikali la SIDO juu ya utengenenezaji wa bidhaa mbalimbali na kufuzu katika hilo nikaona fursa nyingine nje ya kutengeneza bidhaa mimi mwenyewe, nilitambua watu wengi wangehitaji elimu hiyo lakini hawana pa kuipata kirahisi, ndipo nilipoamua kuandika kitabu juu ya mafunzo hayo ambacho sasa kinasaidia wengi kwani mtu anaweza kukipata katika simu yake ya mkononi papo hapo na kuanza kufanyia kazi yale atakayojifunza kwenye kitabu hicho.
Hivo ndivyo unavyoweza kutambua fursa na kuanza kuzifanyia kazi mara moja bila kusubiri kesho; anza sasa, hata kama hakitakulipa leo huwezi jua, inawezekana kesho kikakulipa vizuri sana mpaka ukashangaa.
Ingekuwa hivo leo hii tusingekuwa na facebook kama mwasisi wake angekata tamaa kuanzisha kwa kuwa na wasiwasi wa kupata fedha haraka, na sasa ni miongoni mwa matajiri vijana duniani, whatsapp, twitter, instagram na mitandao mingine, mwanzo haikuwalipa ila sasa dunia nzima inawalipa.
Nachokiamini mimi, hujatumia hata 1/3 ya akili yako, chukua muda na ufikiri utagundua una vipaji vya ajabu sana.
Jipatie copy ya kitabu cha UTENGENEZAJI WA BIDHAA MBALIMBALI ZA VIWANDANI kwenye simu yako kupitia whatsapp kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
Asante kwa kunisikiliza
Ni mwalimu wako;
PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798-Whatsapp
piusjustus28@gmail.com
Page: #THINKBIGSTARTSMALL
PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798-Whatsapp
piusjustus28@gmail.com
Page: #THINKBIGSTARTSMALL
Asante sana kwa kushare.