BINTI NA MAAMUZI MAGUMU YA KUIGWA.

Habari rafiki,  nina imani unaendelea vizuri na mapambano ya kuboresha maisha,  nikutie moyo tu uendelee hivohivo ipo siku Mungu atajibu. 

Kama kawaida yangu kukuletea makala za kukutia moyo kila siku leo nakuletea hii ya huyu dada. 
Nilivutiwa sana na huyu dada na nikapata msukumo wa kuandika hili. 
Anaitwa Asha,  anaishi Dar es Salaam  ni mhitimu wa shahada ya ualimu katika chuo kimoja hivi hapa Tanzania mwaka huu.  Dada huyu ni miongoni mwa watu wanaosubiri ajira serikalini  ambazo mpaka sasa hazijatoka na haijulikani zitatoka lini, mbaya zaidi kuna wahitimu wa miaka miwili sasa,   hii imefanya wahitimu hao kukaa mtaani bila ya kufanya lolote na hatimaye wameanza kulalamika maisha magumu mtaani kwa sababu ajira hamna. 
Nikuulize wewe kijana mwenzangu hivi ikitokea serikali ikatangaza ajira mwaka huu haitatoa utafanyaje? 
Je utaandamana au utafanya nini? 
Baada ya kuona hilo nimekuletea story ya huyu dada ambaye hakuamua kukaa na kusubiri,  anajihusisha na biashara ambazo ziko ndani ya uwezo wake na haumizwi tena na kuchelewa kwa ajira,  hata kama kwa bahati mbaya serikali ikisitisha ajira atakuwa tayari na uzoefu wa biashara yake na maisha yatasonga kama kawaida. 
Cha kujifunza kutoka kwa huyu dada ni:
  1. Tufikiri zaidi ya ajira (think beyond employment) 
  2. Malalamiko hayana tija wala hayatabadili maisha yako. 
  3. Kusoma si lazima uajiliwe. 
  4. Chukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika. 
  5. Kila mtu haijalishi jinsia yako unaweza kufanya mabadiliko. 
Kijana,  siku zote muda hausubiri mtu hata siku moja,  waingereza wanasema time flies,  changamka,  muda ndio huu wa kufanya chochote katika maisha yako. 
Kama huna cha kufanya na umewaza sana umekosa wazo la biashara kulingana na hali yako basi usijari,  kuna zaidi ya biashara 17 ndani ya kitabu kimoja,  naamini ukifanyia kazi moja ya biashara hizo ambazo zinaendeshwa kwa mtaji mdogo kati ya 50,000/- na 100,000/- na kutengeneza faida kubwa ndani ya mwezi mmoja,  nakuhakikishia hutaweza tena kuwaza ajira bali utaweza kutengeneza ajira na kuwaajiri wengine. 

Kupata kitabu hicho bonyeza picha hii  KUDOWNLOAD

Ukifanya moja ya biashara hizo na ukatia nguvu zako zote utatengeneza faida ya zaidi ya 500,000/-kwa mwezi.


Nikutie moyo tu wewe unayesubiri ajira kuwa unaweza kufanya maajabu nje ya ajira,  fanya kama ajira hamna na uanze kufanya chochote kilicho ndani ya uwezo wako,  usiwaze kuhusu mtaji wa mamilioni ya pesa kwa sababu hutaweza kupata,  fikiria kuanza na mtaji kidogo hatimaye utafika kule unakotaka “Think big,  start small” 

Kwa leo niishie hapo,  nakutakia kila lakheri katika maisha yako. 
Wasiliana nasi
Pius Muliriye Justus 
0754745798 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *