MISINGI (3) YA KUWEKA JUHUDI KUFIKIA MAFANIKIO YAKO.

Nafahamu ya kwamba kila mmoja anafanya mambo mbalimbali kama vile kusoma, kufanya biashara, na kutoa huduma mbalimbali. Lakini yote hayo huleta  matokeo chanya  endapo utaweka juhudi za kweli katika endaji wako na kinyume cha hapo utakuwa unashindwa. 
Watu wengi huwa tunafanya vitu ili mradi tu, siyo kama tunapenda kufanya vitu hivyo ila kwa kulazimishwa tu au kwa kuiga kutoka kwa watu wengine mwisho wa siku tunajikuta hatufanyi tena vitu hivyo.
Hebu tuendelee kidogo tuone maana ya neno JUHUDI ni kile kitendo cha kufanya kitu  kwa kutumia bidii, maarifa, nguvu na umakini wa hali ya juu ili kupata matokeo sahihi. Pia juhudi ni maarifa, njia, nguvu ambayo unaipata hata pale wanaokusaidia kwa sasa wakikuucha  je, unauwezo wakusimama peke yako?
Mfano wewe ni mwanafunzi wazazi au ndugu zako wanakusomesha kwa hali na mali, swali la kujiuliza wewe mwanafunzi je una uwezo wa kusimama peke yako endapo wanaokusaidia watakuacha? Je utatumia juhudi gani katika kutafuta njia zako binafsi za kukamilisha jambo fulani?
Ifuatayo ndiyo misingi ya kuweka juhudi katika safari yako ya mafanikio;
Kwanza, Kujitoa.
Ili kuona unapata mafanikio makubwa hakikisha ya kwamba unajitoa kwa moyo wote katika kupata kile unachokihitaji. Kwa kitu chochote unachofanya jitoe kukipenda kitu hicho. Kwa mfano wewe ni mfanyabiashara eneo fulani hakikisha unaipenda kazi yako kwa kujifunza kila siku vitu vipya juu ya jambo unalolifanya. Pia kwa jambo lolote unalolifanya weka juhudi zote na kuhakikisha utapata kile unachokihitaji.
WEKA JUHUDI KWENYE KAZI ZAKO BILA KUCHOKA.
Pili, uvumilivu.
Wengi wetu huwa hatuna chembe ya uvumilivu hata kidogo hasa pale changamoto zinapojitokeza katika mambo tunayofanya. Pia tukumbuke ya kuwa changamoto ni sehemu anayopitia mtu yeyote msaka mafanikio. Jambo la msingi la kuzingatia ni uvumilivu na siyo kukata tamaa. Kuna usemi wa wahenga unasema ‘mvulivu hula mbivu’ Hivyo tuishi usemi huu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzikubali changamoto na kujua jinsi gani ya kuziepuka ili tupate mafanikio tunayoyahitaji.
Tatu, kuwa mbunifu.
Hii ndio siri kubwa katika kutafuta mafanikio makubwa ambayo  yapo upande wako. Kuwa mbunifu katika mambo mbalimbali huku ukiyatendea kazi hayo uliyoyabuni kwa juhudi zote. Kama wewe ni mwanamziki basi fanya kazi hiyo kwa juhudi zote huku ukiamini ya kuwa kipaji hicho ndio sehemu ya maisha yako na kipato chako, usifanye kitu kwa kujaribu.
Katika suala la kuwa mbunifu kuna msomi mmoja amewahi kusema ya kuwa dunia ya leo haitaki kujua wewe una nini ila ioneshe dunia wewe una nini? Nafikiri kwa mfano huo utakuwa umenielewa vizuri zaidi. Pia tukumbuke ya kuwa ubunifu sio lazima kuvumbua kitu kipya bali hata kwa kukiongezea ubora kitu cha zamani pia ni ubunifu pia.
Wapo baadhi ya watu wana pesa  lakini hawana juhudi. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao kumbuka pesa hizo zitakuwa ni za msimu na pindi zitakapoisha utabaki unashanga tu. 
Watalamu mbalimbali wamebaini ya  kuwa na pesa bila  juhudi sio kufikia malengo. Tenda mambo yako katika mtiririko unaoelewaka na ambao unaweza kuutimiza kwa muda muafaka , ukifanya hivyo kuwa tayari kuyapokea mafanikio makubwa.
Ewe rafiki yangu, tukumbuke ya kuwa JUHUDI ndio msingi rasmi wa mafanikio ambayo unayahitaji. Swali la kujiuliza je, upo tayari kulifanya jambo hilo kwa juhudi dhabiti? Kama jibu lako ni ndio basi weka juhudi zako zote katika utendaji wa jambo fulani kwa kuzingatia muda. Ukifanya hivyo mafanikio makubwa yatakuwa upande wako siku zote.
MUHIMU:


Je unapenda kujishughulisha na ujasiriamali???
Kama ni ndio, nimekuandalia kozi maalum kwa ajili yako wewe unayependa kujiongezea kipato.
Kozi hiyo inafundisha jinsi ya kutengeneza batiki zenye ubora mkubwa sana. Kozi hii itafanyika mtandaoni.
Kama unatamani kujiunga basi wasiliana nami whatsapp 0717375782 nikupe maelekezo zaidi.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako.
PIUS J. MULIRIYE
0717375782 | Whatsapp tu.
0754745798 | meseji tu.
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *