MAMBO NANE (8) MUHIMU SANA YA KUFAHAMU KABLA YA KUTENGENEZA BATIKI.

Habari rafiki yangu, naamini unaendelea vizuri na mapambano ya kuboresha maisha yako.

 


Kama ilivyo kawaida yangu nakufunulia fursa mbalimbali ambazo ukiamua kuchukua hatua unaweza kubadili maisha yako kabisa. Cha msingi sana ni kuchukua hatua.

Leo nakuletea fursa ya kutengeneza batiki, fursa ambayo si wengi sana wanaijua kwa maana ya jinsi ya kutengeneza, hata kama watu wanajua kutengeneza bado hawachukui hatua na kufanya fursa hii kuwa ya wachache na imewatajirisha wengi sana na wengine maisha yao yamebadilika kabisa.

Nisikuchoshe sana ndugu, leo hii nakuletea list ya vitu muhimu au mambo manane (8) ya muhimu kuyajua kabla ya kuanza kutengeneza batiki yenye ubora wa hali ya juu. Vitu hivyo ni:-

MAHITAJI:
1.Vibao vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa
7. Jiko.

MADAWA:
8.Sodium hydrosulphate.
9.Caustic soda
10.Mshumaa.

KAZI ZAKE:
1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.
2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.
 
Zifuatazo ni picha za baadhi ya batiki ambazo ninatengeneza na kuwauzia wateja wangu.

 



 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 
Je unatamani kujua kutengeneza batiki?? Hii ni miongoni mwa fursa zilizojificha kabisa na watu hawazioni na hata kama wanaziona hawachukui hatua yoyote, kama unasoma makala hii na unasikia moyoni unatamani kujua jinsi ya kutengeneza batiki hizi basi naamini ndani ya muda mfupi unaenda kuwa mtu mwingine kabisa.

Inawezekana kabisa unajiuliza kuhusu mtaji inagharimu kiasi gani, nataka nikutoe hofu, mtaji wake ni kiasi kidogo saaaana ambacho huwezi kuamini, na utajiuliza kwa nini watu hawafanyi biashara hii kwa wingi na wakati mtaji ni kiasi kidoooooogo sana, nimeshasema sababu hapo juu ni kwamba watanzania wengi hatupendi kujishughulisha, tunapenda kukaa vijiweni kulalamika maisha magumu tu na kuzungumzia maisha ya watu. Ninaamini baada ya kusoma makala hii utakwenda kuchukua hatua mara moja.

Nina habari njema kwa wewe ambaye umependa kujifunza mradi huu.

Kama uko serious na unataka kujifunza jinsi ya kutengemeza batiki basi nimekuandalia kozi maalumu kwa ajili yako.
Kozi hiyo itakufundisha kwa kina, hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza batiki yenye mikunjo/michoro mbalimbali ya kupendeza machoni pa watu.

Kozi hiyo itakuwa kwa njia ya VIDEO ambayo itakusaidia kuangalia kwa vitendo jinsi tunavyokunja mikunjo hiyo na kuweka rangi mbalimbali.

Je uko tayari???

Kama uko tayari niandikie ujumbe whatsapp 0754745798 kwamba uko tayari kujifunza BATIKI kwa njia hiyo kisha nitakuingiza darasani. KARIBU SANA.

Najua bado unajiuliza mtaji ni shilingi ngapi???? Najua vijana wengi tukitaka kuanza mradi flani tunawaza sana kuhusu mitaji. Nataka nikwambie kwa mradi huu hata sh. 15,000/- unaweza kutengeneza batiki nzuri na watu wakabaki kukushangaa. Pia utakuwa unajiuliza nitatoa wapi malighafi???? nataka nikutoe hofu, Tanzania sasa ni ndogo sana, kama hutapata sehemu au mkoa uliopo tutakutumia popote ulipo ilimradi tu utimize ndoto zako. Usiogope, chukua hatua sasa, natamani sana kukuona darasani.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
0754745798| whatsapp tu.
0659908078 | meseji tu (usipige)
piusjustus28@gmail.com
www.piusjustus.com

5 thoughts on “MAMBO NANE (8) MUHIMU SANA YA KUFAHAMU KABLA YA KUTENGENEZA BATIKI.”

  1. Nimefurahishwa sana na mada yako,mm nimejaribu kutengeneza Leo nimeshindwa,nineaandaa vifaa vyote sasa nikifika hatua ya kuchanganya matokeo yake rangi yote inatoka na kubakia rangi nyingine kabisa ya maji sasa hata sijui tatizo nn

Leave a Reply to Pius Justus Cancel Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *